SIFA ZA MTUME WA YESU KRISTO
UTANGULIZI.
🙏Ninakusalimu katika Jina la Yesu Kristo Bwana wetu aliyetununua kwa Damu yake na kutusafisha na Udhalimu wote kwa kufa na kufufuka kwake Hata akashinda kifo na Sasa yuhai milele na Milele.
Kuna Mtu Mmoja Aliniuliza swali kuwa Mitume na Manabii wa Siku Hizi ambao wanajiita Mitume Ni wa Kweli au wanadanganya na Kama Hutaki kunieleza kuhusu Hivyo Basi Naomba nijue Sifa za Mitume kibiblia angalau niwe na Uwanja mpana wa kuelewa Jambo hili Mana natamani kujua Zaidi .
Basi fuatana nami nawe Leo kwa kusoma walau somo hili kwa Utulivu , tafakari na Kutulia ili uweze kujifunza na kuelewa kuhusu Sifa za Mitume na Manabii ukweli kuhusu Kanisa na Huduma zao katika Kanisa na Je Hadi leo wapo au hawapo? Karibu sana
SIFA ZA MTUME WA YESU KRISTO
21 Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu,Matendo ya Mitume 1:21
✍️Aliteuliwa na Yesu Kristo au alikuwa/alimwona miongoni mwa Watu Waliomfuata Yesu Kristo kila mahali alipoingia na kutoka.Matendo ya Mitume 1:21
✍️ Alikuwa miongoni mwa Watu walioshuhudia Huduma Ya Yesu Tangu ubatizo wa Yohana Hadi Kufufuka.
22 kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.Matendo ya Mitume 1:22
✍️Awe Shahid wa kufufuka na kupaa kwa Yesu Kristo.Matendo ya Mitume1:22
Watu wengi huuliza kuhusu Utume wa Paulo aliupataje .Kwanza nikujibu kuhusu Wito wa Paulo .Ni Kwamba aliitwa na Yesu Kristo mwenyewe kupitia Matendo ya Mitume 26:13-18
[13]Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.
[14]Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
[15]Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi.
[16]Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
[17]nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao;
[18]uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Paulo Aliitwa na Kristo Bwana Mwenyewe .na alimpa kieneo maalumu Cha kuhakikisha mataifa Yanamjua Mungu na Mungu Anaahidi Kujidhihirisha kwake .
*15]Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi.*
*[16]Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;*
Kwa Hiyo Mtume Haitwi na Mtu au ajiiti tu .Mtume ana background Yake na Sifa hizo Nne Aina Tatu za Mitume ambao tumewaona Mimi napendaga kuwaita Mitume wa Kweli wa Yesu Kristo..Wale walitengeneza msingi imara wa injili .Sasa Kanisa la YESU Kristo lilijengwa na mitume na Manabii.
Mwamba Ni Yesu Kristo Bwana wetu ambaye Alijenga Msingi pamoja na Mitume na Manabii waliotangulia .walisaidia kuandika na kudurufu Yale Maandiko matakatifu tunayoyatumia Hadi leo hi .Huu Ni Msingi imara ambao Sisi tunaofuatia tunajenga juu ya Msingi huo na ndio Maana Huwezi Kuhubiri habari njema bila kumuweka Yesu Kristo Bwana wetu Kama kiini cha Injili , injili ya Uweza ,maajabu ,upako ,Nguvu ,Uponyaji ,Baraka Kama haijawapelekea Watu kukiri na kumwamini Yesu Kristo kwa hiari moyoni mwao Basi hio sio injili .
Sifa za Nabii huyu Mpya anazitoa wapi ,ili aandike Nini ,kwa kusudi la Nini .?
*11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; Waefeso 4:11*
*12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; Waefeso 4:12*
Kama Hujaona faida ya hizi karama 5 za Huduma Basi leo jua Mitume na Manabii walijenga Msingi wakatuachia Sisi tulijenge jengo husika.Kama leo hujajengwa na Nyaraka za Paulo,Petro ,Yohana,Marko ,Mathayo,Luka .au Manabii wadogo na wakubwa , Historia nk Basi ndio Maana unaamini kuwa Hadi leo Kuna Nabii na mrume yumkini ujaweza Kuhusianisha ukweli huu .
Mtume Paulo na Petro wote wawili walitupa Siri zote za nafasi Yetu Sisi katika Kanisa pale tu tunapookoka.
🙌🙌Nafasi ya Kwanza katika Kanisa alisema miili Yetu Ni Hekalu la Mungu (Kanisa).Maadamu Roho Mtakatifu anaketi ndani Yetu Basi sisi tu Makao Yake na tu Hekalu lake Takatifu .
*Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?1 Wakorintho 3:16*
*Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.1 Wakorintho 3:17*
neno ninyi linamaanisha Watu /kikundi /wengi (uwingi wa Mtu 1) Lakini Roho Mtakatifu anaishi ndani Yetu pale tu tunapoamini .kwa Hiyo Kanisa na lijulikane kuwa Waliomwamini Kristo kuanzia Mtu Mmoja Mmoja Hadi kundi au kusanyiko la Mhubiri wa Neno la Mungu anaposoma Maandiko matakatifu na kuyafafanua kwetu huo.sio Ufunuo mpya kwa Namna ya kwamba Amepewa Moja kwa Moja kwa kuvuviwa na Mungu Bali amesoma Kutoka Neno la Mungu na kufafanua ili sote tuelewe Yale Mungu alionena na Watu kipindi kile yalimaanisha Nini na Sasa pia yanamaanisha Nini hasa ili tuweze kutekeleza (kutii).Tuamini kuwa Hata Mafundisho ya Musa ,Daudi nk Yanatujenga Hadi Sasa 😊
🙌🙌🙌.Mtume Petro anafafanua Tena Zaidi nafasi ya Mtu Mmoja katika Kanisa yaani Mwili wa Kristo.au Hekalu la Mungu .kuwa hatujui sisi Ni Matofali (Mawe) ebu tuanzie kwenye Maneno ya Yesu Kristo Bwana wetu.katika Mathayo
*Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.Mathayo 16:18*
Mwamba Ni Yesu Kristo.ambao Mitume na Manabii waliweka Msingi wao katika Mwamba na ndio Maana Yesu aliwaambia yeyote ajengaye nyumba juu ya Mwamba mafuriko yajapo hayataweza kubeba nyumba Yake Mana itakuwa juu Tofauti na Yule ajengaye ndani ya Mchanga .
*Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.Luka 6:48*
Mimi nimekubali kuwa nitajenga juu ya Mwamba katika Msingi uliojengwa na Mitume na Manabii.Yani Nitawajenga wengine kwa Mafundisho Ambayo Kiini chake kitakuwa Ni wao waweze Kumfuata na Kumtii Yesu Kristo Bwana kwa kutumia Maandiko matakatifu yaliotoka kwa Mungu mwenyewe kupitia Kwa Mitume na Manabii waliokatibu Biblia.Ukifanya Hivyo Hata Wewe ndugu yangu katika Kristo Yesu Bwana wetu hautaweza Kujenga juu ya Mchanga na Msingi mbovu.kumbuka
*Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.Waefeso 2:20*
👆👆👆👆Mimi na wewe leo Ni Mawe Muhimu yaliotafutwa na kuchongwa na Mungu mwenyewe ili yaweze Kujenga Hekalu lake Takatifu .Petro amekazia Zaidi Sisi tuna asili ya familia ya Ufalme wa Mungu, Ukuhani Mtakatifu,Taifa Teule la Mungu.1 Petro 2:5-10
*5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. 1 Petro 2:5*
*6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.1 Petro 2:6*
*7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.1 Petro 2:7*
*8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.1 Petro 2:8*
*9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;1 Petro 2:9*
*10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.1 Petro 2:10*
Hallelujah kumbe Basi Neno la Efeso
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.Waefeso 2:20
Tunalielewa Zaidi kwa kupata kufahamu kuwa kila Aliyemwamini Yesu Kristo (Aliyeokoka) Ni Jiwe katika Kujenga Kanisa ,Yesu Kristo Ni Jiwe kuu la pembeni (Mwamba imara) Sisi sote tunajua bila Jiwe Moja kuu la pembeni ndipo tunapoanzia kusetia nyumba Yetu na vipimo vyote vinaanza kuchukuliwa kuanzia Msingi ndipo nyumba nzima.na Mitume na Manabii ndio Msingi wenyewe(Foundation) Ambayo nyumba ikijengeka hapo inategemea Mwamba ilioukalia na Msingi husika na Matofali yaliyotumika .
Hallelujah kwa Hiyo kwenye level ya Matofali yatumikayo Sasa Sisi ndio tunajenga juu ya Mitume na Manabii waliotangulia kujenga katika Mwamba imara Yesu Kristo Bwana wetu.
Mitume na Manabii wa Kweli Walituandikia Maandiko Matakatifu Ambayo Ni Msingi Hai wa kuratibu kuujenga Ufalme wa Mungu kwa kutumia Neno la Mungu waliloliandika kwa kuvuviwa na Roho Mtakatifu.
kumbuka Hakuna Ufunuo mpya kwetu ambao utatoka nje ya Maandiko matakatifu.labda Kama watoka kwa Shetani Biblia inatuambia Kuwa Maandiko matakatifu Ni Ufunuo Kamili kabisa na inatuasa kutohangaika kutafuta mafunuo mapya sawasawa na Neno la Kumbu Kumbu la Torati 29:29 .
*Yasiyofunuliwa Ni Mungu pekee na Yaliyofunuliwa Ni Yetu Sisi na Watoto wetu*
kwa Hiyo Basi Amini ya Kuwa Siku hii akikuambia Mtu Nabii Basi yeye ni Nabii wa Agano la kale sio Jipya lenye shauri la Roho ,na Bado yupo kimwili Sana na kazi ya Mwili Ni Uongo ,tamaa ,ushawishi ,udanganyifu na Ukosefu wa ustahimilivu na Uvumilivu.
kumbuka Neno la Mungu ndio Ufunuo Kamili Hakuna Ufunuo mwingine tuupasaokuuamini isipokuwa Neno la Mungu litokalo katika Maandiko matakatifu kwa sababu zifuatazo 🤔🤔🤔
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.Waebrania 4:12
✍️Lihai
✍️Lina nguvu
✍️Lina ukali kuliko Upanga ukatao kuwili
✍️Ni Moto uchomao
✍️Linatambua Makusudi na mawazo ya Moyo.
sababu nyingine Muhimu Sana zipo katika waraka wa Kitumishi (kichungaji ) upatikanao katika 2Timotheo 3:15-18.
*15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.2 Timotheo 3:15*
*16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;2Timotheo 3:16*
*17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 2 Timotheo 3:17*
✍️linatuhekimisha Hata kupata wokovu
✍️Linatufundisha
✍️linatuonya makosa Yetu
✍️linatuaongoza
✍️linatuadibisha katika Haki
✍️linatukamilisha katika kutenda kila Tendo jema .
Mwenye Sikio 👂na Asikie .👂👂👂
MAWASILIANO
0764141648
Harakati ya kufanya wafuasi wa Yesu Kristo Tanzania (HKWY-TANZANIA)
Kuwafanya wafuasi wa Kristo wanafanya wengine kuwa Wafuasi wa Yesu Kristo.
Kwa seminar za Uanafunzi wa Yesu Kristo tupigie kupitia namba hizo hapo juu.
0 Comments
Post a Comment