*MFANO WA MZAZI MWAMINIFU*


*Utangulizi*


Ninakusalimu katika Jina la Yesu Kristo Bwana wetu ambaye ametufadhili na kutuneemesha pumzi ya uhai mpakatumeiona Siku ya leo.

nimaombi yangu kwamba umzima wa Afya tele .Karibu Tena Leo tujifunze Jambo Moja Muhimu Sana kwa Maisha Yetu Kimwili na Kiroho kuhusu kuwa Mzazi mwenye uhusiano Mzuri na Mungu (Mzazi Mwaminifu).


Ayubu Ni Mmoja Kati ya Watu ambao waliishi katika nchi ya Usi na alijulikana Sana mbele za Mungu ,alikuwa Mtu aliyeneemeshwa na Mungu Kwa kuwa na Mali Nyingi hasa Mifugo mingi lakini Mungu hakumtambua kwa Hayo .Mungu alimtambua Kama Mtu Mkamilifu mwelekevu na Mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu.


Sasa ebu tumuangazie Ayubu Kama Mfano wa Mzazi mwenye uhusiano Mzuri na Mungu (Mwaminifu).



KICHWA:MFANO WA MZAZI MWAMINIFU


*NENO*    

*Ayubu 1:5*


*[5]Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.*



1.✍️Anamtanguliza Mungu kwenye Familia yake .Ayubu Alifanya ibada maalumu Kwanza aliwatakasa Watoto wake .aliona si vema kufanya karamu nyumbani mwake ilingali hajui kuhusu wanaye na jamaa zake Kama Ni wasafi au laa  .*akawatakasa* .


*Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa* ,


Je Wewe unamtangulizaje Mungu .Ayubu Alifanya Kama Yesu alivyofanya kwa wanafunzi Wake akawatawaza Miguu ikiwa Ni ishara ya Kuonesha kuwa Wanahitaji kusafishwa. Pili Jambo lile linaonesha Jinsi Mungu atupendavyo Watoto wake Hata akamtoa Yesu Kristo ili tuweze kusafishwa /kutakaswa kwa Damu ya Yesu .


Jinsi Ayubu alivyojari na kuwapenda Watoto wake akawatawaza ndivyo Tukimuamini Yesu Anatufanya wanae anatutawaza kwa Damu Yake tunakuwa wasafi hatuna dhambi Tena ..Amini tu .Mzazi Mzuri huipenda na kuijali familia Yake Kama Mungu atujalivyo na kutupenda .uwe Mzazi Bora . Mwamini Yesu.na Uwapende na kuwajali wanao 🙌🙌🙌🙌🙌


2.✍️Anamshukuru Mungu /Anajitoa au kujitolea kwa ajili ya Wanaye 


*..,kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa;...*

Ayubu alitolea sadaka mbele za Mungu kwa ajili ya kila mwanae Tena Asubuhi na mapema Mana anatambua kuwa Fadhili zake Bwana huwa Nyingi na mpya Asubuhi .

Jinsi Ayubu alivyonisaidia kwa ajili ya wengine ndivyo Mungu Wa Mbinguni akajitolea Yesu Kristo Bwana wetu ili awe sadaka ya kuteketezwa (Sadaka ya ondoleo la uovu /dhambi kwa ajili Yetu tupate kufutiwa hatia)

Unaweza Kuamini Jambo hili Muhimu Sana Kujua Mana Yesu ndiye  Aliyejitolea uhai wake kwa ajili ya kukufadhili upate kuokoka Je uko tyr! kuokoka?


3.✍️Anadumu siku zote katka kuomba Rehema na Msamaha kwa ajili ya Wanaye/Watoto wake.


Mzazi anaye mjali Mwanaye huomba rehema na Msamaha kwa ajili ya Watoto wake.sikiliza Ayubu alijua asili ya Mwanadamu Ni uovu na asemaye hanadhambi ajidanganya mwenye NDIYO Maana aliomba Rehema kwa ajili ya Watoto wake.


*...,Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.*


Ayubu Ni Mfano wa Mzazi Mwaminifu ambaye anaomba Rehema kwa ajili ya wanawe Nasi Tukimuamini Yesu Kristo Bwana wetu tunafanyika Wanaye .Tukifanya dhambi Yesu Kristo anatuombea anafanyika mwombezi kwa Mungu .


Maana yake Ni nini Mungu Ni Mzazi mwema na Mwaminifu


Anajali ,Anatupenda anataka tuishi Milele endapo tu tutamwamini Yesu kuwa ndiye aliyefanyika sadaka yakuondoa makosa na dhambi zetu kwa kufa na kufufuka KWAKE .


🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻


Je Wewe Ni Mzazi Mwaminifu?


✍️ Mwamini Yesu uokoke

✍️Wapende na kuwajali Watoto wako

✍️Waombee Rehema Watoto wako kila Siku.

✍️ Mshukuru Mungu kwa ajili ya familia yako kila siku.


Ninatummaini utaishi Mapenzi ya Mungu.


Mungu akutunze , akusaidie na akupe neema hiyo Zaidi .



(Ukiokoka )Ukiamini na kutii utauona Uaminifu wa Mungu Maishani mwako.


MAWASILIANO YA MTUMISHI

@Petro Malele

HKWY TANZANIA

0764141648..