*NDUGU WANAHESHIMIANA KATIKA KRISTO*


1 Petro 3:8

[8]Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Watu wanaoheshimiana ni wasikitivu na wanyenyekevu.watu wanaoheshimiana Ni watu waliostarabika..


Petro anawaandikia Watu ambao wapo ktk Mahangaiko ,Dhiki ,na msteso makali Kuwa waaipoteze Ustarabu wao kama Watu wake Kristo Bwana wetu yaani wawe Ni watu walio ndugu .Yani Watu waliozaliwa Mara ya pili kwa Njia Ya Yesu Kristo Bwana wetu.ambao Ni watu


1.✍️wenye Nia Moja 

2.✍️Kuhurumiana

3.✍️Kupendana 


1.✍️wenye Nia Moja 

Nia Moja Ni Kuwa na shauri moja,lengo Moja ,ono Moja , Mpango Mmoja wa Kristo Kwanza na mengine badaye .

.Watu wanaomwamini Yesu Kristo Ni watu ambao Mtazamo ,fikara na falsafa Ni Kama ile ya Kristo Yesu.watu wenye umoja katika imani huamini Jambo Moja na kusema kauli Moja .


*Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.1 Wakorintho 1:10*


Kumbe lengo la Kristo halikuwa sisi.kuwa na rangi.tofauti za makanisa Bali Kuwa na makanisa yenye rangi Moja .kwa mantiki hio basi Kama nia Yetu Ni Imani katika Kristo Yesu Basi tumwishie Yeye Milele .na sio kufuata Mila na desturi.Mfano Kuna Watu wanasahau kwamba Kanisa sio Jengo Ni Uwepo wa Yesu Kristo katika Kusanyiko haijalishi namba na isipunguwe Wawili . Yawezekana  Wewe na Roho Mtakatifu tayari mnasifa ya Kuwa taswira ya Kanisa kwa sababu Mungu Yupo hapo na ibada inaendelea.lakini akiongezeka Mtu Mmoja Ni Bora Zaidi .Kutaniko lolote lenye uwepo wa Yesu Kristo Bwana lenye lengo la Kuonesha utukufu wa Yesu Kristo Kama Mwokozi wetu Kati ya wanakusanyiko haijalishi mahali gani nje ,shimoni ,na sehemu kedekede madam Uwepo wa Mungu upo Kanisa Hilo.Binadamu Ni Hekalu la Mungu .Sasa Nia ya Kristo Bwana Ni kuhakikisha ufalme wake unaenea Ulimwenguni mwote.Mathayo 28:18-20.



2.✍️Kuhurumiana

Tabia kubwa ya Mungu Ni Huruma .Maana Yake si Mwingi wa hasira,Ni mwenye Rehema ,mpole na mkweli.


Kutoka 34:6

*[6]BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;*


kwa Hiyo Kwa Kuwa Sisi tumekuwa Wana wa Mungu tunapaswa Kuhurumiana Sisi kwa Sisi .Na Mungu pia atazidi kuziachia Huruma zake kwetu .samehe Mtu akukoseapo,mpende akuoneae na mpende Adui Ni Moja ya kumhurumia kwani Mungu hakumuumba Mwanadamu kwa kusudi baya Bali jema .


*Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.Warumi 9:15*


3.Kupendana 

Upendo ndio utimilifu wa sheria .bila Upendo Mwanadamu Ni kitu bure .Mungu mwenyewe alitupenda Sisi alipimtoa Mwanaye Wa Pekee afe kwa ajili ya dhambi zetu(Yohana 3:16 ) Maana Yake Ni Yesu Alitupenda tungali wenye dhambi (waovu,wachafu ,tusiyostahili,tusiofaa,tukiwa tumeharibikiwa) kwa Hiyo ni nani miongoni mwetu anayejidai kuwa Hawezi kuwapenda wengine? Basi itakuwa Ni wakakini Ya kwamba mtu asiyempenda nduguyo au wa Kwao Hawezi kuwapenda Adui na Watu wengine.


Biblia inatuhimiza Sana kupendana Kama ndugu katika Yesu Kristo Bwana wetu.upendo ninaouzungumzia Ni Huu ambao Mtume Paulo alisema hauthamanishwi kwa mtu kuwa na Mali,kushika dini au dhehebu lake,kunena kwa lugha ,kuimba mpaka unasifiwa au kufanya maajabu bila Upendo Vyote Hivyo Ni bureee Bali Upendo Huu upo katika Yafuatayo


*Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;1 Wakorintho 13:4*


*Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.1 Wakorintho 13:8*


kumbuka.


*Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.1 Yohana 4:20*


Kuna Muda huwa nasema hivi kuwa Haiwezekani unaomba kila Siku Adui ateketezwe ,akatwe afyekwe wakati Yesu alikuja kwa wapotevu ,wenye dhambi na Anasema Wapendeni Adui zenu 🙌🙌 tunawafyekaje tuwapendao .utasikia wafedheheke na kufutiliwa mbali hatuwatakii Mema unakuta Ni Kanisa Jirani unawaita watesi


Mungu atusaidie Sana .Heshima ya Kimungu Ina Nia ya Kristo,inahuruma na inaupendo .ndani Yake .


Tuyaishi Hayo Mambo Matatu tusiwe wenye Nia Mbili Hatuwezi kutumikia mafahali wawili .tusipohurumiana Hatuwezi kusameheana na tusipopendana Hatuwezi kukaa pamoja .ili Tuwe Pamoja ktk Kristo Tunahitaji  Tuwe  na Nia Ya Kristo ,huruma ya Kristo na Upendo wa Kristo ndani ya Mioyo na Masha Yetu yaakisi Mambo haya Muhimu kwetu sote .

*Mwenye sikio na asikie*


@Petro Malele

0764141648

HKWY-TANZANIA


*Harakati ya kufanya wafuasi wa Yesu Kristo wanaofanya wengine kuwa Wafuasi*.