*Mtumishi Anayekubalika na Mungu.

1️⃣.✍️Hutumia Neno la Kweli kwa Usahihi 

2 Timotheo 2:15

[15]Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.


kutumia Neno la Mungu kwa Usahihi huonesha jinsi Ambavyo Mungu anakuwezesha Wewe Kujua Siri zake (kibali) ,inaonesha kwamba hautahayari ,hauogopi ,hauna Shida 


2️⃣✍️ Huchunga Usemi wake 

2 Timotheo 2:16-18

[16]Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,

[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

[18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.


〰️Hazungumzi Maneno yasiyo ya Maana (yasiyo ya Dini)

〰️Hapindui usemi -Haenezi habari Mbaya ,Habari chafu ,Habari ambazo hazifai 

〰️Haenezi Imani ya Uongo

〰️Haukumu Wengine kwa sababu Anayejua siri za Wanadamu wote Ni Mungu .Anamuachia Mungu Kuweza kufanya Kazi ndani Yake na ndani ya wengine.

2 Timotheo 2:19

[19]Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake.Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.


2 Timotheo 2:19-22

[19]Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, 

Bwana awajua walio wake. 

Na tena, 

Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.


3️⃣✍️Ametengwa na Mungu mwenyewe kwa Ajili ya Kazi Yake Maalumu(Yupo kwa sababu ya kuyatimiza Mapenzi ya Mungu)


〰️Mungu amekutenga kwa sababu anajua wewe Ni chombo chake unafaa kwa mahali ulipo na kwa Kazi Hiyo .


[20]Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.


〰️ Mungu amekutenga anataka uwe  na  Moyo Safi yaani uache Tamaa ,ufuate Haki Imani Amani na Upendo na kushirikiana na watakatifu.


[22]Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.


4️⃣✍️Uwe Mwanana kwa Mwenendo Mzuri kwa Watu wote .

〰️Epuka Ugomvi na Usiwe mgomvi 

〰️Fundisha Neno la Mungu

〰️Uwe Mvumilivu 

〰️Onya kwa upole ili Watu watubu na kuijua Kweli


2 Timotheo 2:24-26

[24]Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;

[25]akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli;

[26]wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.


*Hitimisho*


✍️Uwe Mwanana kwa Mwenendo Mzuri kwa Watu wote

✍️Ametengwa na Mungu mwenyewe kwa Ajili ya Kazi Yake Maalumu

✍️Hutumia Neno la Kweli kwa Usahihi 

✍️Huchunga Usemi wake 


❤️Tumejifunza haya Ili Sisi sote tuzidi kubadili Fikara zetu katika Bwana Yesu Kristo ili Tuweze kuwa watumishi na mawakili wazuri wa Kristo popote tuwapo


❤️Tumeweza kujifunza ili tuweze kufahamu Kuwa Mtumishi Mwema anapaswa kuaje .

p kujifunza ili tujue ukweli kwa Nini Mungu ametupa uwezo Tofauti katika kutenda Kazi ya Mungu.


❤️ Tumejifunza ili tuweze kuwa na Ushirika mwema na kufuata Yale Ambayo watumishi waaminifu waliotengwa na Mungu wanapoyawasilisha kwetu kutoka Neno la Mungu.


Kwa Hiyo itoshe tu kusema 1Timotheo 4:15

*Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote*


 Ahsante Mwenye sikio na Asikie 🙏