BIBLE STUDY KITABU CHA ZABURI 

ZABURI
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Zaburi 1:1

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Zaburi 1:2

3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. 
Zaburi 1:3

4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Zaburi 1:4

5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Zaburi 1:5

6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. Zaburi 1:6


Tabia ya Mungu 
✍️ Mungu anatujua Jinsi -6
✍️Bwana Ni Mwenye Mamlaka na Haki (Mwenye sheria Haki) -6
✍️Bwana Ni Mwenye Mamlaka na Haki (Mwenye sheria)-2
✍️ Mungu ndiye Mfadhili wetu.


Tabia ya Mwanadamu

Maisha ya Dhambi
✍️kufuata Mambo yasiyo ya Haki (Mvunja sheria)-1
✍️Mkosaji -1
✍️Hupendelea Mzaa_1
✍️Hatendi Haki -4
✍️Hafuati Neno la Mungu (sheria ya Mungu-4
✍️Mtenda dhambi/Mkosaji atahukumiwa na Mungu 5
✍️Hataweza Kuingia katika kusanyiko la wenye 5 Haki Kama Ni mwovu au mwenye dhambi(Hataokolewa)/hataingia Mbinguni-5
✍️Anapotea katika njia ya wakosaji -6

MAISHA Matakatifu
✍️Asiyefuata wasio Haki (Atendaye Haki)-1
✍️Asiyesimama katika njia ya wakosaji (Asiyependa njia ya Uovu au wakosaji)-1
✍️Asiyeketi barazani pa Wenye mizaa.(asiyefanya mizaa)-1
✍️ Anapenda Sheria ya Bwana (Neno la Mungu) -2
✍️Anatafakari Neno la Mungu-2
✍️Akitii Neno Mungu Atafanikiwa katika Kila Alitendalo (Hufanikishwa na Mungu)-3
✍️Anaokolewa na Mungu (Atakusanyika katika kusanyiko la wenye Haki -Watakatifu)-5
✍️anajulikana na Mungu kwa kufuata njia  ya Haki  -6


UTII 
Je unadhani Ni tabia Gani Ambayo Haipo sawasaw na Mungu unahitaji kurekebisha ,kufuata na Kuendelea kufuata katika maisha yako?

kumcha Bwana Ni kuacha dhambi na kumwamini Bwana /Mungu wetu .

Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wetu .Tunapaswa kumwamini Kristo na kuhesabiwa  haki bure kwa Imani katika Yeye .hapo Tutakuwepo katika kusanyiko la wenye Haki.

Je unahitaji kujua Jinsi ya kuacha dhambi na kumwamini Kristo Bwana.ni Rahisi tu 
0764141648 kwa mawasiliano Zaidi 
@HKWY Tanzania.