HUPASWI KUOGOPA!
Bwana ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako; Hutaogopa uovu tena. Sefania 3:15 
Kwa Nini Hupaswi Kuogopa❓ 
✍️Bwana Ameziondoa Hukumu zako
✍️Amekuokoa kwa kumtupa Adui nje
✍️Bwana Yupo nawe 
Kama Mungu alivyofanya kwa Wanna wa Israeli walipokubaliwkumwamini na Kutubu dhambi zao katika kipindi kile ambapo Hasira ya Bwana iliwaka juu yao Je Rhemea zake zimekwisha sasa? je Mungu anaweza kufanya katika Maishe Yestu leo ?🤔

Jibu Ni NDIYO 
Mungu anaachilia Rehema zake na Neema Yake kupitia Yesu Kristo katika Maisha Yetu .

Ukimwamini Yesu Naye Anakusamehe,Anakuokoa ,Anakuwa nawe milele .AMINI LEO UOKOKE upate Uzima wa Milele na kuwa na Uhusiano wa kuwa Naye Milele.

Wewe Unamwamini Yesu Kristo?
Je Ni kitu gani kinakuzuilia wewe usimwamini ? Je Ni dhambi,Ni shida ,Ziki ,Taabu , Uchumi wako au mmeo au dini yako ? 
Nataka nikwambie kuwa Hakuna kitu kinaweza kututenga na Upendo wake Kristo wa kutusamehe kutuokoa na Kuwa Naye kea sababu Kristo hakai mwilini Anakaa Katika Roho yako Kwanza kabla hayajaanza kutokeaMatokeo ya nje Atakupa Hekima ya kuacha na kukiondoa kile kikutengaye Naye ..

Omba Sala Hii Kisha Tuma Namba yako ya simu Nikuombee kwa kumwamini Kristo awe Bwana na Mwokozi wa Maisha Yako (Kuokoka) yaani Aakusamehe dhambi zako zote ,akuokoe na Kuwa nawe Milele).

FUATISHA MAOMBI KUTUBU👇👇
Bwana Mungu mbinguni Ambaye uliwasemehe Wanna Israeli walipokutenda dhambi na ukawaokoa na kuwa pamoja nao .Mimi Leo nimeamini Neno lako ninaomba Unirehemu na kusnisamehe Mimi kwa kutenda dhambi ikiwepo ile ya asili tangu adamu kupitia Yesu Kristo Bwana na Mwokozi .unisafishe niwe Safi kwa damu ya Yesu ,ninaomba uovu na dhambi zangu usizikumbuke .Bali uandike jina langu katika Kitabu Cha Uzima wa Milele..Ninakushuru kwa kunifadhili Namna Hi Ameni.


Kwa Kuomba na Kusoma Sala Hii AMINI kwamba Umesamehewa dhambi zako zote ili kuthibitisha Kiri kwa Moyo na kinywa chako kwamba kweli Alikuja ili wewe upate kuokolewa kwa kifo chake sisi tumesamehewa ,tumeokolewa na Tutapata uhusiano na Mungu Milele.Amen.

Wako Mtumishi Petro James Malele M.
@HKWY Tanzania.
Harakati ya kufanya wafuasi Tanzania
0764141648.
Kama unaona umeokoka piga simu Nikuombee 🙏🙏🙏🙏.