KUCHUNGUZA MAANDIKO.✍️✍️✍️

Yohana 5:39-42
" Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu."

 Leo nataka tuone dhima ya Bible study (Kuchunguza Maandiko na Matokeo ya hayo Maandiko)

lmekuwa kila siku tukisoma Neno katika vipindi Vya Bible study kuanzia fellowship, Makanisa na Hata Majumbani lakini .Nini dhima ya Bible study .

Kwa Nini Tunachunguza Maandiko 
✍️ Maandiko yanashuhudia habari za Yesu Kristo
✍️Ili tuweze Kumtii /Kumwamini Yesu Kristo (Tupate uzima wa milele)
✍️Ili Tuzidi Kukua katika Upendo wa KiMungu.
✍️Mtu kibinafsi aweze kutakaswa kwa kulifuata Neno linapomwagiza
✍️Ili Mungu Atukuzwe.

Kwa Hiyo dhima ya Bible study yoyote inalenga kuleta Mabadiliko binafsi ndani ya Moto wa Mtu anayesoma Maandiko hayo Ili aweze kuokoka, Kuendelea kumwamini,Kukua katika Upendo na kujua Jinsi ya Kumfuata Yesu Kristo.

lakini Yesu Ametoa angalizo Kuwa Kusoma Neno la Mungu/Maandiko sio ili Tuwe na Maarifa Mengi yasiotekelezeka Lahasha .

Kuwa na Maandiko mengi hakukufanyi Uonekane Umekua Kiroho Bali Kuyatii hayo Maandiko ,kuyafuata na kuwashirikisha katika Upendo hayo huzaa Matunda Mema .hii ndio dhima yake.

Lengo la Kusoma maandio sio Mambo yafuatayo.

✍️Kuwa na Maarifa Mengi yanayokosa Utii
✍️Kuwa na Maarifa Mengi yanayokosa utekelezaji wa Kiimani 
✍️Kusoma Sana halafu Haujaokoka au kutakaswa na Neno Hili
✍️Kusoma Neno hakukupi uzima wa milele 😊 Bali kumwamini na kumkiri Yesu Kristo kutakupa uzima wa milele baada ya kusikia Neno Hilo Vema 😊
✍️Kusoma Neno Bila kulitii au kulifuata hakumpi Mungu utukufu ✍️Kusoma maandiko hakumaanishi Unampenda Mungu Bali kuyatii na kuyatumia Maandiko katika maisha yako na ya wengine kunaonesha unamtii na kumpenda Mungu .

kumbuka 🤔

15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 
2 Timotheo 3:15

16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 
2 Timotheo 3:16

17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 
2 Timotheo 3:17


✍️Ukisoma Maandiko matakatifu Kwa Lengo la Kumtii Mungu Kwanza na sio Kuwa na Maarifa Unaweza kuongozwa nalo,kuadibishwa nalo,kurekebishwa nalo ,Kukaripiwa nalo .pia Utajengeka katika Kumfahamu Mungu na Yesu Kristo Bwana Wetu.katika kufanya Hivyo Uhusiano wako na Mungu Utaongezeka zaidi .


🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏:

Tuwe na dhima na dhamira au Nia Njema ya kuyasoma Maandiko matakatifu kwa minajili ya kujua Jinsi ya kumpendeza Mungu na sio Wanadamu .Maana Mungu anatambua Yote Hata yaliyo Siri.

Tumuombe Mungu atusaidie.Mana Neno lake Ni takatifu lafaa Sana Kulishika kwa Utakatifu uleule.

Badilisha Nia Yako na Mtazamo wako Neno la Mungu laweza kukuhekimisha Hata Ukapata wokovu.Amini tu  inawezekana.

@Petro Malele
HKWY Tanzania.
0764141648-whatsaap/Text  nk