Uhuru Uletwao na Kristo ktk Maisha Yetu

Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.Yohana 8:36 

Mambo muhim ya kujua katika Andiko hili

✍🏾Kabla ya Kuwekwa huru (Hauko Huru ,umefungwa,Upo mahabusu ,Upo kifungoni ,unatumikishwa ,umefungiwa)
✍🏾Kuwekwa Huru -kutoka katika kifungo ,kuwa na Uhuru au uwezo wa kuamua mwenyewe ,kukosa Kifungo au kuondoka kifungoni
✍🏾Baada ya Kuwekwa Huru .hapa Ni Uhuru wa Uhakika .Maana Yake Ni Hauko chini ya Magereza Bali chini ya Wewe mwenyewe.kuwa Huru kweli kweli .

🙌🏻Mwana Ni Yesu Kristo 

✍️Kabla ya Kuwekwa huru Ni Maisha ya Dhambi ..Maisha ya uovu,yaliyojaa Tamaa na kutojizuia ,kua chini ya uongozi wa mwili na nafsi ,kuwa chini ya Ubinadamu wako.

👂Bila kuwa na Yesu Kristo mwili unaweza kukupelekesha utakavyo ,kukuendesha utakavyo,Tamaa za mwili zitakuendesha zitakavyo ,dhambi itakuvizia na uovu utakukumbatia , Udhalimu utakuwa fungu lako,Dini itakukamata na kukusumbua ,unakosa utambuzi  yaani utakuwa umefungwa,uko Chini ya sheria 

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Yohana 8:34
👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.Wagalatia 3:23
👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆

imani gani Hiyo ije Soma hatua inayofuata👇

✍️Kuwekwa Huru.ni Kumwamini Yesu Kristo Bwana wetu ambaye alituokoa Kutoka katika vifungo vya dhambi,Tamaa ,uovu nk.na kutusamehe na kutuweka katika ufalme wake.

Ni Hali ya Kuwa Chini ya uongozi wa Yesu Kristo Bwana wetu.."Mkiwa na Yesu(mwana) mtakuwa ....."

*Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini),Warumi 10:6*

*Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.Warumi 10:8*

*Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Warumi 10:9*

 *Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.Warumi 10:10*

*Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.Warumi 10:11*


✍️Baada ya Kuwekwa huru./Maisha baada ya Kumwamini Yesu (Kuwekwa huru).Haya Ni Maisha ya kuongozwa na Roho 

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.Warumi 8:9
👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆

.Ni Maisha ya burdani Ni kuwa na furaha na shangwe Wakati wa Mgumu na mepesi,kuwa na Uhusiano na Mungu Moja kwa Moja huitaji kuhani kupaingia patakatifu ,Yani unao ujasiri wa kupaingia patakatifu Muda wowote kwa Jina la Yesu Kristo (Mwana) Wakati ukiwa hujamwamini Kristo Bwana wetu kibali hicho Hakuna mpaka kuhani awepo Naye Ni Yule aliye na Mwana Tu.


Je Umemwamini Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa Maisha na uhai wetu .? Je Umemkiri ?Je Upo nae? 

Tambua Uhuru wa kuwa na Mwana Ni ile Roho Mtakatifu anaingia kwako pasipo uyo Roho Mtakatifu katika Maisha Yetu hatuwezi kuwa Huru . Mwamini Yesu Kristo uwe Huru .

*Basi ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru*  2 Wakorintho 3:17


Kama Hujamwamini Kristo Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako ninakusihi kwa Huruma zake Mungu mwenyezi kuanzia Sasa Amini na Kiri kuwa Yesu Ni Mwokozi wako anayechukua hatia ya makosa yako Yote na Dhambi ya asili iliyoanzia pale bustani ya Eden kupitia Baba Yetu Adamu .

Pili Uliyemwamini Yesu Kristo Jaribu kuongozwa na Roho Mtakatifu na Maandiko matakatifu yanayokuongoza kila Siku ,Adibika ,rejebika ,fundishika na Onyeka Kisha ongozeka kwayo .

Usisahau Kuwafundisha wengine usisahau kutangaza habari Njema za Yesu Kristo Bwana wetu ili ufalme wake Kristo uzidi kuenea myoyoni mwa Watu wapate kuliamini na kulikiri Jina lake.kuwa ni Bwana na Mwokozi .

Anakupenda Yesu Kristo ananipenda Sana pia . Tuendelee kuwashirikisha wengine Habari Njema .

wako katika Kazi ya Mungu 
Petro Malele
Huduma ya HKWY-TANZANIA.
Harakati ya kufanya wafuasi wa Yesu Kristo Tanzania.
0764142648