NENO LA LEO :MHUBIRI 1:16-18
KICHWA: MOYO WANGU SIKILIZA ❤️👂
Utangulizi Mfupi
Kitabu Cha MHUBIRI Ni mojawapo ya Vitabu muhimu katika Kujifunza.
Kwa kiebrania Mhubili husomeka Qoheleth na kwa Kiyunani Ecclesiastes.Neno Mhubiri tafsiri yake Ni "Mwalimu".
Kitabu Hiki Kinafafanua zaidi Upi hasa Ni "UMAANA WA MAISHA" kikionesha Ubaya wa kushika Shughuli za Kidunia Kama Kazi ,fedha,Elimu,Mali,Maarifa,busara,hekima za kibinadamu ,ujuzi kuwa hazina manufaa yoyote Kama Kumcha Mungu .Sulemani Anatumia Neno Ubatili mtupu na kujilisha upepo akimaanisha kwamba Hakuna kitu chochote duniani kina Maana zaidi ya Kuishi kwa kumtegemea Mungu.
Ebu tujifunze Sulemani Alivyoweza kuuambia /kuwaza Moyo wake na kutambua Mambo ya Msingi Kama ifuatavyo
KICHWA: MOYO WANGU SIKILIZA ❤️👂
Sulemani Aliuekekeza Moyo Yake kwa kufanya ,kugundua na Kuweza kufanya Mambo Matatu Ambayo tutayaona leo kwa kila Mtu kuuambia moyo Sikiliza
1 ✍️Mtafakari Mungu na Ujifunze kwake
16 Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. Mhubiri 1:16
Sulemani mwandishi wa kitabu Hiki Alikuwa Ni mtu alijaliwa Hekima na Maarifa mengi (Alijenga hekalu bila Shaka Alikuwa na ujuzi wa Kiinjinia😊).Alikuwa na Elimu kubwa kuzidi Watu wote ,Alijifunza Vitu vingi Sana .Maana Yake Ni Nini Jaribu kutumia Hata Part ya Muda wako kujifunza Mambo yanayoongeza Hekima na Maarifa bila Shaka namaanisha Soma Neno la Mungu Sana .
Sulemani Hekima na Maarifa hakuyapata kwa Mwanadamu Bali alipata Kutoka kwa Mungu MWENYEWE .Kwa Hiyo tukitaka Kuwa na Hekima na Maarifa ya kweli tusome Neno la Mungu pekee.
2.✍️Tambua kuwa Kujua/Kuwa na Hekima na Maarifa mengi bila Kutii Ni ubatili na kujilisha upepo.
17 Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo. Mhubiri 1:17
Mungu akikupa Maarifa na Hekima Anataka uitumie kwenye Maisha Yako ya kila Siku na kumrudishia yeye Utukufu katika Mambo Yote yatendekayo kutokana na Maarifa au Hekima Hiyo.Kuwa na Maarifa mengi Sana akafu utiii kidogo na Huwezi kuwaambia wengine na kuwatumia kwenye Maisha yako Basi jua Ni Ubatili mtupu.
Hatujifunzi Kumjua Mungu kwa Kusoma Biblia na kuwa na Maarifa mengi Sana ya kibiblia lakini Huyatii na kuyaishi hayo Maarifa uliyonayo Basi ndipo tunaita Tragedy (Hatari mbaya) . Sulemani anasema inakuwa Ni Ubatili mtupu na kujilisha upepo tu .
Mungu alitupa Neno lake ili sisi tuweze kuyaishi Mapenzi Yake Kinyume na Hapo tunapoteza Muda .Ndio Maana Imani chanzo Ni Kusikia na inahitaji kuzalisha Matendo yenye Mapenzi ya Mungu ndani na nje .Imekuwa kasumba kubwa ndani ya Maisha Yetu kusoma Neno Sana na kuwa na Maarifa mengi na kuacha Utii na Kuishi na Kushirikisha Yale tunayoyaishi au kuyatii tumebaki tu Kama tulivyo Hakuna matunda yoyote yanayotokea .
Kuwa na Neno la Mungu kichwani Sana hakumaanishi unayajua Bali umejalili kuyaishi na kutenda sawasawa na Neno la Mungu Ni kutimiza Mapenzi ya Mungu hili ndilo kusudi kuwa Tuwe na Uhusiano na Mungu wa Mbinguni.
🤔Jitahidi kuyaishi Yale unayoyasoma na kuyatii Yale ya kweli uweze kukuza Imani yako ,Utii Ni Bora kuliko Dhabihu/sadaka 👈👈👈👈
✍️Tambua kuwa Furaha hailetwi na kuwa na Maarifa au Hekima Bali Yatoka kwa Mungu .
18 Yaani, Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni,Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko. Mhubiri 1:18
Hili Ni Jambo Muhimu kujifunza hapa Mana Watu wengi wamekutwa katika masikitiko na huzuni kutokana na Elimu Yao ,Ufahamu waliokalilishwa na kufundisha.alafu ndani ya Maarifa yao hayajawasaidia Kama watakavyo.kinachobaki Moyo huumia .Mithali Moja imeandika kuwa "Moyo ukikosa Uyatarajiayo unaumia" 🙌🙌🙌
Elimu , Maarifa mengi Sana ya Neno la Mungu, Hekima yako mwenyewe na kila Ujuzi ulionao hauwezi kutufanya kuwa Sisi na Furaha ,Amani na Upendo kwa muda murefu Kama sio Mapenzi ya Mungu .
Tunasoma maandiko ili tuweze Kumcha Mungu katika Maisha Yetu.Tukifanya Kinyume na Mungu Basi twafanya kwa Mapenzi Yetu wenyewe..
Mungu anatosha na Maarifa Yake yatiosha kukufanya uuone Ufalme wa Mungu ukiyatii na kufuata Kama Atajavyo .
Maisha bila Mungu Ni Bure .Kabisa .
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔😊😊😊Sasa Basi Mambo hayo Sulemani Alijifunza kwa kipindi alipowaambia wanna Israeli Je Kwetu Sisi leo yanamaanisha Nini ?
✍️Tutafakari maandiko na Hekima zetu.
✍️Tutambue kuwa UMAANA wa Maisha hauletwi na Maarifa au Hekima Bali Utii katika Neno la Mungu na Kuishi sawasawa na Na Mungu anavyosema katika Neno lake na sio kuwa na vifungu vingi bila kuviishi.
✍️ Kutambua kuwa Elimu tulizo nazo au Maarifa tuliyonayo kama hayajaelekezwa kwenye kumpa Mungu Utukufu,Kumjua na Kumtii yeye na kutumika kwa ajili ya Utukufu Heshima yake basi hazina Faida Bali zinaleta huzuni, masikitiko
mfano Vijana wengi tumejikutaga tunalakamika Hatujapata Ajira tunailalamikia serikali Yetu .🤔Je Ushawahi kutumia Maarifa na ujuzi huo kibinafsi na Kuweza kutekeleza sawasawa na Ujuzi wako?
kama unaona hujawahi na haiwezekani ndivyo Mungu anavyolalamikiwa na Watu ambao wanadhani wanastahili kupata Vitu ,kitu na Kuomba Kupewa kwa sababu ya Maarifa na Ufahamu wao bila kuyaishi Yale Maarifa Ambayo Mungu Ameweka Mapenzi Yake na tukiyaishi tu Kuna Matunda yake tutayaona na yatatupunguzia Huzuni na masikitiko na malalamiko zaidi Tutakuwa na Furaha na Amani Katika Maisha Yetu.
Yesu Kristo Bwana ndiye Neno la Mungu lenye uzima ukikubali kuliamini ,Kutii na kumfuata Utaoana furaha katika kila ulifanyalo .maandiko haya yalionesha Kazi Ya Yesu katika Maisha Yetu.mafarisayo walishika sheria na ikawa ndani Yao na Maarifa na Kila ujuzi lakini walishindwa kutambua Mapenzi ya Mungu kwa Kudhani Maarifa mengi Sana ndiyo utakatifu kumbe Ni Ubatili mtupu na kujilisha upepo.
inuka umwamini maana Kamwe Hiyo Elimu ,fedha ,Mali na Ujuzj wako haviwezi Kukupa furaha na Amani ya kweli Ni ya Muda ikipita katika Mambo magumu,shida na magonjwa itakufa Bali ukiwa na Yesu unayo Milele kwani Hata yakikupata hayo unajua kwa Hakija Yesu yupo nawe kila wakati na Anataka uone Mapenzi Yake katika Magumu pia .
je Unapenda kumwamini Yesu Kristo?. Tafadhari hima wasiliana nami kupitia email jamesmalelesigala@gmail.com
0764141648
Mungu Akubariki.Amen.
0 Comments
Post a Comment