MUNGU NI MWINGI WA FADHILI Zaburi 106:44-46

Katika Zaburi ya 106,107 , Zaburi hizi zote Mbili zinaeleza zaidi kuhusu wema na Fadhili zake Mungu katika Maisha Yetu.

Kwanza zinaanzia kuekeza matukio makuu ,Matendo makuu aliyoyafanya Mungu katika Historia ya Taifa la Israeli Mungu alipikuwa akiwaongoza Kutoka Kule Misri Kupita katika Jangwa Hadi kufika Kanaani .inaonesha Jinsi Mungu alivyowafadhili wakiona njaa,kiu,mbele ya Watu waliowajilia kuwaangamiza,walipotenda dhambi akawarehemu ,walipotangatanga katika miaka 40 hile wakatoka na kufika Kanaani Bado Mungu Alikuwa akionesha Fadhili zake .

walipita katika Dhiki ,Shida ,taabu na katika Mambo mengi magumu Mungu hakuwaacha alionesha wema na Fadhili zake aliwasaidia .

Ebu leo tujifunze katika mistari hii ya Zaburi 106:44-46 tuone Mungu alioneshaje Fadhili zake kwa kipindi Kile na kipindi Hiki Yani kwetu tufanye Nini au anaweza kutufadhilije?

44 Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao. Zaburi 106:44
45 Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake; Zaburi 106:45
46 Akawajalia kuhurumiwa Na watu wote waliowateka. Zaburi 106:46

Kichwa :Mungu Ni Mwingi wa Fadhili
Mungu Ni Mwingi wa Fadhili kwa kuwa 

✍️Anatazama Mateso na Kusikia kilio chako 
"Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao." Zaburi 106:44

✍️Anahurumia Wateswao na kumlilia
"Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake; " Zaburi 106:45

✍️Anasaidia na kuondoa Mateso.
 
"Akawajalia kuhurumiwa Na watu wote waliowateka." Zaburi 106:46

Mungu Kwa Fadhili zake Aliwatazama Wana Israeli katika Mateso waliyoyoyapata na kwa kilio walichomlilia akawahurumia akawasaidia kuwaondoa katika yale Mateso walipokuwa Chini ya Utumwa wa Farao .Sasa kwetu Sisi leo Neno hili linatufundisha Nini ili tufanye Nini ?

Moja Tutambue wana wa Israeli walilia sababu wakipitia Mateso makali Sana Ambayo Mateso hayo kwa leo inaweza ikawa Ni dhambi ,Uchungu wa Moyo utokanao na kutengwa ,kudharauliwa ,kuugua magonjwa yasiopona ,inaweza ikawa Ni Maisha magumu Maana yake hivi Vitu vinakufanya kuwa kana umetekwa huoni Pakutokea Kabisaa nataka nikwambie Kitu 

Moja ✍️Mlilie Mungu juu ya Jambo Hilo linalotesa Maisha Yako
Mbili ✍️Tambua Mungu mwenye Fadhili atakuhurumia kwa wkt wake 
tatu ✍️Tambua Mungu anaweza na atakusaidia kukuondoa matesoni .

Mungu Ni Mwingi wa Fadhili atakufadhili ,Atakuona , atakuhurumia na KUKUSAIDIA Jaribu kusimama upya Tena katika Maisha Yako kumbuka Yesu Kristo Bwana wetu alipokuja Alitutazama katika dhambi zetu akiwa Mbinguni akalia kwa Uchungu kwa sababu aliona Jinsi dhambi inavyotutesa katika Maisha Yetu Wanadamu akaja kwetu akiwa ametuhurumia ili atukomboe katika dhambi ikampasa auvae Mwili wa Kibinadamu ili  afe kwa ajili ya Kulipa Deni kwa Damu Mana Hakuna Ondoleo la dhambi bila kumwaga damu ,Damu yake iliyomwagika pale msalabani ilitosha kufuta Mateso Yetu ya Dhambi zinazotesa Maisha Yetu endapo tu tutakubali Kuamini na kukiri kuwa Yeye Ni Bwana na Mwokozi wa Maisha Yetu .

Je Wewe Umemwamini Kristo?
Mateso =Dhambi zako 
Kilio=Toba yako mbele zake
Msaada wa Mungu=Wokovu .

Kuokoka Ni Sawa na kupokea Huruma za Mungu katika Maisha Yetu ndio Maana Twasema sio Sisi Bali Ni Neema ya Mungu Ni kwa Huruma za Mungu Sisi Tumeokolewa .
Mwamini Yesu leo na Kumkiri utapata Wokovu .

✍️✍️✍️Fadhili zake Mungu zibazihilika kwetu leo kupitia Yesu Kristo Bwana wetu ambaye Ametufadhili Sisi Wanadamu kwa kutupatia Wokovu endapo tukiamini na kukiri kwamba Yeye Ni Bwana na Mwokozi wa Maisha Yetu.

Mungu Akubariki.
kama uko tayari kuokoka.nitasikia ukiri wako kupitia 0764142648.
@HKWY-TANZANIA 
Up Rev Petro Malele.