UFALME WA MUNGU MFANO WA MKULIMA WA NGANO.🕎✝️

26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;Marko 4:26
27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Marko 4:27

28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Marko 4:28

29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.Marko 4:29


✍️Mtu Aliyepanda Mbegu =Mungu wa Mbinguni
Mbegu Ni Neno la Mungu
Nchi (Udongo) Ni Mwanadamu asikiaye Neno la Mungu na Kukua katika Hatua mbalimbali
kuota hadi Jani Ni Hali ya mbegu(Neno ) kuingia ndani (ardhini) na kuota (Kupokelewa) na kutoa Jani Ni Kuokoka .

✍️Teke (Uchanga wa Wokovu) -Katika Hali ya Kwanza ya Kukua Kiroho MKristo hufananishwa na Jani teke kwani anahitaji Kupewa virutubisho stahiki Kama mtoto mchanga wa Kiroho . Virutubisho hivyo Ni Mafundisho ya  Neno la Mungu lisiloghoshiwa.Moja ya andiko linasema  

"Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu ;" 1 Petro 2:2

SUKE Ni hatua ya pili ya ukuaji wa Mmea ambapo majani yanapata uwezo wa kujitengenezea Chakula chake na Kukua.
Maana Yake Ni hatua Ambayo Mtu aliyeokoka ametoka kwenye Hali ya kufundishwa mafundisho ya Neno la Mungu kwenda kwenye hatua ya Pili ya Kumtegemea Mungu na kujifunza kupitia Neno la Mungu.
katika hatua hi Mwamini anapaswa kumsikiliza Sana Roho Mtakatifu katika Kujifunza Neno la Mungu ili Kuweza kukuza imani yake na kusababisha matunda Ya Roho Mtakatifu kutokea.

✍️Ngano Pevu katika suke 
Baada ya kusoma Neno na akilitii na kulifuata Neno la Mungu huzaa matunda Ya Roho Mtakatifu(Ngano Ni matunda ya Roho Mtakatifu) Ambayo huanza kumomaa ,Kukua kutegemea kadri Mwamini anapozidi kuwa Mwaminifu katika kulisoma ,kulisikia Neno ,kutii na kuwajibika kwa Neno Hilo au kutii kufuatana na linavyomwelekeza .Kisha kuzaa Kisha kukomaa katika kuzaa matunda na kuwa tayari kwa Mavuno .

katika Hatua ya kuwa tayari kwa Mavuno Ni hatua Ambayo Hata Paulo Alisema "hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;Waefeso 4:13

👷Mwenye Mundu ,Mundu ,Mavuno 
Mwenye Mundu=Mungu
Mundu=wavunao (Malaika)
Mavuno=Wanadamu waliomwamini Kristo na kuzaa matunda ya Roho Mtakatifu na yaliokomaa.(Ngano).

Yesu Kristo Bwana wetu atarudi Tena kunyakua wote waliomwamini Kristo na Kuzaa au Kuishi maisha ya Utakaso katika kutii na kulifuata Neno lake.

🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🏻🙌🙌🙌🙌🙌swali langu wewe Umemwamini Yesu Kristo?
Wewe uliyeokoka Ni Mtu wa hatua gani Yesu Kristo akitudi leo? Je Ni Teke,suke,Ngano komavu juu ya suke?

Jani likipitiwa na ugonjwa linakufa 
Teke likikosa Virutubisho hufa (Mwamini akosae Neno hufa Kiroho)
Suke likikosa Kuendelea Kutengeneza Chakula na kupata Virutubisho hukosa kuzaa kabisaaa 

🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
🙏Je wewe Ni Jani,suke au ngano iliyokomaa?

👂Ebu Ambaye hujaokoka)humwamini Kristo kuwa anasamehe dhambi zako zote na Kukupatia uzima wa Milele.Yeye Ni Mwokozi wako?
Mwamini Leo upate Msamaha wamaovu Yote na uzima wa Milele(Wokovu).

👂Kama wewe Ni Jani Tafuta kujifunza Neno la Mungu Kutoka Mafundisho mbalimbali kwa watumishi waaminifu wasiofundisha Uongo.

👂Kama wewe Ni Suke jitahidi kuzidi , kujifunza Neno la Mungu na kutafakari,kulitii na Kuzaa matunda ya Roho Mtakatifu.

🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
kumbuka Ndugu Yangu Yesu Kristo Bwana wetu Atarudi-Maranatha atakukuta upo Namna gani?

Mungu anisaidie na akusaidie wewe pia.