MKRISTO KATIKA KANISA LA KWELI NI YUPI?

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
 Ufunuo wa Yohana 2:7

Mambo Matatu ya Kujifunza

👂👂👂 KUSIKIA NENO LA MUNGU
💪💪💪USHINDI KATIKA KRISTO
🙌🙌👐KUPEWA UZIMA WA MILELE

Kitabu Cha Ufunuo Ni Moja ya kitabu cha Kinabii pekee katika Agano Jipya.Kimeandikwa Na Mtume Yohana Akiwa katika Kusiwa Cha Patmo ,Kikigusia mazingira ya Makanisa 7 na Waumini Ulimwenguni kote katika Kuwaasa kusimama katika Imani ya Kweli ya Siku na kuwatahadharisha kuhusu kuja kwake Yesu Mara ya Pili.

kitabu hiki kiufupi kimechukua asilimia Kubwa ya Maandiko ya kuanzia mwanzo ,kutoka na Vitabu vingine vyote vya Agano la kale Kuweza Kuweka bayana kuhusu Uungu na Uwepo wa Yesu Kristo Kuwa Alikuwepo tangu Mwanzo ,Aliyepo sasa na Atakayekuja Tena.....niishie hapa kwenye Utangulizi !

Maandiko Yanasema

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
 Ufunuo wa Yohana 2:7

Katika Kanisa la Efeso Ni Moja ya Kanisa lilopatikana Asia .ambalo Sifa zake lilikuwa Ni Moja ya Kanisa lililozingatia Nidhamu ,lisilopenda injili ya Uongo ,linalopinga Uzushi ,lilishikilia injili ya Kweli ,Kanisa lilikuwa na Uvumilivu mkubwa na SUBIRA . kiukweli lilikuwa Ni Kanisa lilikuwa linawapima Hata Mitume waliokuwa wanahudumu pale na watumishi wake kulingana Na Neno la Mungu linavyosema .lakini Kasolo ilikuwa miongoni mwa Watu au Waumini wake Ni Kupoa Kwa Upendo .

Mungu anawaambia kwamba Watubu Hiyo Ni dhambi na Wakitubu  Bwana anatoa Ahadi ya kwamba mwenye 👂 KUSIKIA na Asikie lakini Atakayeshinda nitampa matunda ya uzima wa milele

 🤔 Kumbuka.Sifa Hizi hazikuwa lile Kanisa (jengo) lahasha Bali Waumini wake mmojammoja  ndiyo walikuwa na Sifa Hizo .

KWA Hiyo neno Hili Ni Neno ambalo limetoka Moja KWA Moja KWA Mungu likituitaji na Sisi leo Kanisa(Watu wote Duniani tunaomwamini Kristo Bwana wetu Kama Mwokozi wa Maishani Yetu) kuzingatia Mambo haya 3.

1.👂👂👂 KUSIKIA NENO LA MUNGU
Kwanza Mungu akisema "Mwenye Sikio na Asikie Ambayo Roho ayaambia Makanisa" 2:7a Anamaanisha Waumini tuchague Kama tunanwaminj kweki tusikie na Kulifanyia kazi Neno lake linalofundishwa na kunenwa kwetu .kupitia Maandiko matakatifu na Watu waaminifu wanaoihubiri injili .
kuwa Watu wenye Upendo ,wavumilivu,wenye Saburi ,wenye kupinga Uongo katik injili unaoletwa na watumishi wasiowaaminifu,Kukubali Yesu Kristo Kuwa Bwana wa maisha Yetu,Kupima Mafundisho ya Watu wanaojiita Mitume ,Manabii waongo na wenye kupotosha ,kutochukuliana na Watendao Mabaya (Kusimamia Nidhamu ya Kanisa kisawasawa)

Kama nikisikia Sauti inaniambia Tubu na Acha dhambi nikaipuuzia Basi Mimi siwezi kutakasika kwani Uchafu utakuwepo ndani Yangu Milele.Jamani Ndugu zanguni Tumsikie Mungu na Kumtii.


2.💪💪💪USHINDI KATIKA KRISTO
".........,Yeye Ashindaye ......"
katika Maisha Yetu Waamini tukikubali Kuacha dhambi na kusimama Katika Kweli ya Yesu Kristo kwa kuwezeshwa na Yesu Kristo mwenyewe,  Basi Tambua kuwa Sisi tumeshinda na zaidi ya kushinda Tena kule Kushinda kuushindako Ulimwengu.Ukiamini Yesu Ni Bwana na Mwokozi wako unakuwa umeshinda lakini ukisimama na Kristo na kumfanya akuwezeshe na kutawala Maisha Yako Basi umeshinda Tena .yaani umeshinda na zaidi ya kushinda .


3.🙌🙌👐KUPEWA UZIMA WA MILELE
"........ . ....,nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu."

Yesu Anaahidi kuwa Kila Mtu aliyeshinda yaani Aliyemkili Yesu Kristo Bwana na Kuamini kuwa Alikufa na kufufuka na kufutilia Mbali hatia ya dhambi yako jua AMESHINDA lakini Akiishi Maisha ya Utakaso akimfuata Yesu Kristo kwa kuwezeshwa na Kristo Bwana wetu Kikamilifu na kwa uaminifu na si Akili au Vitu vyetu ,thamani nk   AMESHINDA na Zaidi ya Kushinda.Thawabu mbele zake Mungu Ni tofauti Sana na Yule ambaye Ameokoka lakini Hajasimama katika Kuishi Maisha Ya Utakaso na Kuongoza na Mungu mwenyewe.

Yatupasa Kusikia na Kuamini injili ,Kisha Kutubu tunapoona tupo kinyume katika Maisha ya kila asikiaye Neno Kisha Kurekebisha mwenendo na fikara Yetu .na kuendeleza Kufanya sawasawa na Neno la Mungu lisemavyo .Hapo tutashinda dhambi (uovu ) .Tutapata Uzima wa milele Siku ile Yesu Kristo Bwana wetu Akirudi Kumlipa Kila Mmoja sawasawa na Kazi Yake ilivyo .

wako katika Kazi ya Kristo
@Up Rev Petro Malele.
HKWY-TANZANIA
0764141648.
Harakati ya kufanya wafuasi wa Yesu Kristo.

Mungu akubariki kwa Kujifunza Jambo hapa karibu Tena kesho kwa Tafakari nyingine .Amen 🙏