NAFASI YA NENO LA MUNGU
Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki;upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. Kumbukumbu la Torati 6:1-3
Neno la Mungu ndani yake limebeba mambo mengi lakini makubwa ni amri ,sheria(kanuni/Maagizo) na Hukumu/ahadi .Mungu ametupa Neno la Mungu maisha mwetu ili tuweze
kumtii Mungu ili tufanikiwe
kumcha Yeye ili tuweze kukua katika kuhusiana na yeye na kulngezeka.
Kifupi ni kwamba katika kulitii na kumwabudu Mungu sawasawa na neno lake tunapata kufanikiwa na kukua katika kuhusiana na yeye katika maisha yetu ya kiroho na kimwili.
Sasa ili Neno la Mungu litiiwe vizuri tunahitaji Mwalimu kama Musa alivyoagiza kuwakumbusha wana wa Israeli nga'ambo ya Yordani ambao baba zao walikataa kutii Mungu Kule Masa wakaangamizwa .sasa kizazi hiki cha Israel hakikujua vizuri kuhusu Mungu alivyofanya. Kwa Taifa zima la Israel.
Musa anaambiwa Uwafundishe Neno la Mungu (sheria ,amri na Hukumu) za Mungu ili wapate kunitii na kuniabudu .Kwanza nikomee hapo nirejee kwako na mimi ndugu .Je Mimi nawewe tunajifunza Nini kupitia somo hili?Nina uhakika kuwa mimi na wewe Tunahitaji neno la Mungu ili tumwabudu Mungu na kumcha Mungu na kumtii Mungu na sauti yake .
Mara ngapi tumekuwa na moyo wa kufundishika.????
Moyo wa kufundishika umebeba mambo 2
Utii na ibada ya kweli
Utii na ibada ya kweli hutawaliwa na Roho Mtakatifu pekee imebeba uhuru ndani yake .
Moyo usilfundishika umebeba
Kiburi
Ibada ya sanamu
Kiburi na ibada za sanamu zinatawaliwa na mapepo au Shetani mwenyewe.
Tahadhari
Uchaguzi wa wapi umeamua kuwa unategemea umeketi wapi na hatua utakayoichukua .
Kutohudhuria Ibada ni kuchagua kutofundishika .mara nyingi kunasababishwa na Shughuli za kifedha ,mali ,uvivu ,kutokwenda na muda na kutojitamalaki .hizo ni ibada za sanamu .nina uhakika kama Mungu hajakupa ridhiki asubuhi hadi muda wa vipindi vya jioni hawezi kukupa kwa masaa 2 au 3 ya ibada ya jioni .kikubwa ni kukosa imani .Mungu anafanya kwa wakati wake .panga muda na jipe imani atafanya ukimtii na kumwabudu hata kwa iyo biashara au kazi yako.Kuchagua kutojifunza au kutofundishika ni kuchagua laana na kuchagua kumtii Mungu na Kumwabudu ni kuchagua baraka
Neno linasema
Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana;baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo leo;na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua. Kumbukumbu la Torati 11:26-28
Kile unachochagua maishani kinaathiri maisha yako .
Mwaka huu 2022 amua kwenda na Bwana .
Amua kumtii Mungu
Amua kumwabudu Mungu
Amua kuokoka
Ishi na Bwana uwe na Moyo wa kufundishika.
Kuwa na Moyo wa kufundishika ni kumpenda Mungu wetu .
4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Kumbukumbu la Torati 6:4
5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Kumbukumbu la Torati 6:5
Kuwa na Moyo wa kufundishika ni kuwa radhi kuwapa au kuwafunza wengine Ulichonacho kwani Mwanafunzi Mzuri ni yule anayesikia ,anatii na kusambaza kile anachojifunza .
Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.Kumbukumbu la Torati 6:6-9
LIPE NAFASI NENO LA MUNGU.LIKUKUZE,LIKUSTAWISHE.
Pastor Petro Malele
0764141648
Karibu Tegeta Azania Tumwabudu Mungu wa Kweli.
0 Comments
Post a Comment