KAZI YA ROHO MTAKATIFU KWA KILA ALIYEOKOKA

1. kuwafananisha waumini na Kristo Warumi 6:3-4 Wakolosai 2:12

‘’Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?, Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.’’  Warumi 6:3-4

2. huokoa Roho Mtakatifu ndiyo njia ya Mungu ya kutekeleza kuzaliwa upya ndani ya - muumini,huzaliwa upya au kutoka juu. Tito 3:5 Yohana 1:12-13 Yohana 3:3-8, 1 Kor. 6:11

si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. Tito 3:5

3. hutakasa na kusafisha dhambi Roho Mtakatifu hushiriki katika mwenendo wa utakaso kutokana na dhambi. Warumi 2:29, Warumi 8:13-14

kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Warumi 8:13-14

4. huweka wakfu na kutakasa Warumi 15:16 , 2 Wathesalonike 2:13, 1 Petro 1:2

Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli. 2 Wathesalonike 2:13

5. huishi kikamilifu kwa daima Roho Mtakatifu huishi daima ndani ya muumini. Yohana 3:34,  Yohana 14:17,  1 Kor. 6:19,  1 Kor. 3:16,  Warumi 8:9

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. 1 Kor. 6:19

6. uthibitisha na kudhamini wokovu Waumini wote wanahifadhiwa na Roho Mtakatifu aliyetolewa kama mdhamana wa hatima ya wokovu wetu. 2 Kor. 1:21-22 Waefeso 1:13-14 Waefeso 4:30.

Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. 2 Kor. 1:21-22

7. huhakikisha wokovu Roho Mtakatifu, ki-ndani, hutushuhudia sisi kwamba tu watoto wa Mungu. Warumi 8:16

Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu. Warumi 8:16

 8. hutujaza ili tuwe na uwezo na huduma Roho Mtakatifu, huelekeza, hutamalaki na kushawishi waumini. wanaokubaliana naye. Waefeso 5:18

Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu. Waefeso 5:18

9. huzaa matunda ya tabia ya Kristo katika maisha ya muumini Wagalatia 5:16; 22-25,Wagalatia 6:7-8.

Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. Wagalatia 5:16; 22-25

10. huangaza fikara ziweze kuelewa na kukubali mambo ya Mungu 1 Kor. 2:10-15, 1Yohana 2:20, 27

Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni,. 1 Kor. 2:10-15

11. huwaombea waumini kulingana na mapenzi ya Mungu. Roho Mtakatifu huwasaidiawaumini katika udhaifu wao. Warumi 8:26-27 Waefeso 6:18

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Warumi 8:26-27

13. huwatambua roho wa uwongo na dini za uwongo Roho Mtakatifu huwawezesha waumini kutambua kweli na uwongo. 1Yohana 4:1-4

Wapenzi, msiiamini kilaroho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. 1Yohana 4:1-4

14. Huelekeza na kuongoza Roho Mtakatifu huwaonyesha waumini mwenendo mwema wa kuishi. Warumi 8:14

Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu, Warumi 8:14

15. hufundisha waumini ukweli Yohana 16:12-15

Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

 Bwana Yesu Kristo Apewe sifa ,Ninapenda kukualika kila wakati kutembelea blogu hii na ili kupata taarifa zako please follow bolgu yetu ya harakati za kufanya wanafunzi wa Yesu Kristo(HKWY) 

 Wenu Mzee wa Kanisa la Kristo na Kiongozi wa Huduma ya HKWY Tanzania 

Contact 0764141648 

Email :petrojamesmalelesigala @gmail.com