MUNGU NI MWAMINIFU MILELE
Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote. Sefania 3:19

kitabu Cha sefania ni Moja ya Kitabu Cha kinabii katika maktaba iitwayo Biblia Ambayo Nabii Sefania aliandika akiongozwa na Mungu mwenyewe.
Kitabu Hiki kinaeleza Uasi uliofanywa na Wayuda na Israeli na Utabiri juu ya ghadhabu ya Bwana Juu Yao lakini Kama wangali Tubu Mungu Anatoa Ahadi yake ya kuwasamehe na Kuwarehemu .

✍️Katika Siku ya leo tunaweza kusema kitabu Hiki kinaelezea Wokovu katika Picha kubwa Yaani Hali ya Dhambi na uharibifu Ndani ya mioyo ya Watu na Maisha yao ,Injili ya Msamaha iletwayo na Kristo mwenyewe na Kuamini na kugeuka kufuatana na injili uliosikia ..

Leo tunajifunza katika Sefania 3:19
kuwa Mungu anaahidi kuwatunza Watu wote wanaomwamini na kumtegemea Yeye .Kama ifuatavyo

Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote. Sefania 3:19


Mambo ya Kujifunza
✍️Mungu Anaahidi Kuwapatiliza/kuwaadhibu wote wanaokutesa ktk Maisha Yako

✍️Mungu ndiye mponyaji wako atakuponya majeraha yako ya Moyo .Anajua Siri Zako zote as longer Hata ukiumia Moyo ,umechanganyikiwa kivipi ,umeachwa ,umeumizwa ,umetekekezwa .Mungu Anajua na  anaahidi Kukuponya )kukuganga . Mtegemee tu .

✍️Mungu atakurudisha katika Mahali upofukuzwa .Najua kipindi kile Wanna Israeli walipelekwa utumwani na wajateseka .Ilikuwa Ni wkt Mgumu Kwao lakini Leo hi Mungu Anajua Shetani na Ubinadamu wako umekuweka Mbali na Yeye oooh anaahidi kukurudisha Tena .
Najua Kuna mahali ulikuwa katika kila nyanja ya Maisha yako lakini Baada tu ya kuachana na Mungu ukaporomoka huna mbele Wala nyuma na huelewi ufanye Nini .My dear let me tell you Mungu atarehesha vyote Mwamini,mtumaini na mtegemee.aliahidi kurejesha Hata Miaka iliyoliwa na nzige na madumadu atashindwaje kwako leo hiii 👈.Usijali Amini to utauona uweza wa Mungu Maishani Mwako.

✍️Mungu atajitukuza kupitia Wewe .Atakuinua kutoka fedheha Hadi Sifa ,kutoka zero Hadi Hero,kuto kuchoka kuchakaa Hadi upya na kung'aa.Mungu atakufadhili na kukuwezesha atakutia Moyo ushindwapo ,atakuwezesha ukwamapo Amka Tena haijarishi Hali yako ukiamini tu utaona Makuu na Kwa kufanya Jambo lolote ukimshirikisha Yeye Utatenda Makuu .Maana Kwa Msaada wa Mungu tunashinda na zaidi ya KUShINDA.

Ndugu Yangu Unadhani una Jambo gumu linaloweza kukushinda ?Basi Mpe Yesu

Je Unatambua ukitumia Ubinadamu (Akili yako,fikara Zako, feeling nk) haziwezi kukufanya ukashinda Bali Ukimtegemea na Kuamini Mungu anakuwezesha utakuwa Mahindi Daima .

Mwamini Yesu Kristo leo .Kwa Msaada wake Utatenda Makuu .

Amani , Furaha na Upendo Katika Kristo Yesu na Vidumu Milele Amen .

@Petro Malele
HKWY-TANZANIA
0764141648