SADAKA YA KWELI @Rev Petro Malele

Somo la tarehe :1 Wakorintho 16 : 1-24 ;



16.1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.  16.2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
2 Wakorintho9:6-8
9.6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. 9.7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. 9.8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

Mambo ya kujifunza
Ø  Mungu ni Mtoa Riziki kwa kadiri ya Neema yake –mstr 2 Wakorintho9:8
Ø  Mungu ni wa Neema-mstr 2 Wakorintho9:8
Ø  Mungu anapenda watu watoe kwa Moyo wa Ukunjufu-mstr 2 Wakorintho9:7
Ø  Mungu anataka tuweke akiba ili tuweze kumtolea Mungu.mstr 1 Wakorintho9:1
Ø  Mungu anapenda tutoe kwa ukarimu –Mstr 2 Wakorintho9:6
Ø  Tunapaswa kumtolea Mungu kwa kadiri ya kufanikiwa kwake mstr 2 Wakorintho9:2
Kanisa tunapaswa
Ø  Tuwapende watu na kuwakarimu
Ø  Tutoe sadaka kwa ajili ya Huduma
Ø  Tufanye huduma gani ambayo itahitaji tutoe na kuwasuport wengine?
o   Yatima,
o   Wajane
o   Machoraa-watoto wa mitaani
o   Wasiojiweza
o   Kuwatunza wajane
Inabidi kanisa litazame huduma hizi katika jicho lake la kufanya huduma ili kuwaleta watu wa kila aina kwa Yesu Kristo .