TAFAKARI YA MATHAYO 1:1-17


Mathayo 1:1-17

 

Kitabu cha Ukoo wa Yesu Kristo Mwana wa Daudi,Mwana wa Abrahamu

 

Yesu Kristo ni kutoka ukoo wa Daudi

Kwa nini?  ukisoma unabii wa nabii Nathani ,nabii aliyetumika kipindi cha mfalme Daudi alimwambia Daudi unabii kutoka kwa Bwana kuwa mwanaye atakayezaliwa kutoka kwake (ukoo wa Daudi) -Yesu Kristo  

·      Atakuwa Mfalme atakayerithi kiti cha Enzi cha Daudi na 

·      Utawala wake utakuwa Imara 

·      Atajenga Nyumba ya Mungu(Kanisa)

·      Kiti cha enzi yake kitakuwa cha milele

·      Ataitwa Mwana wa Aliyejuu(atakuwa mwanangu nami nitakuwa baba yake)

·      Upendo wa Mungu kwake hautaondolewa(mwanangu mpendwa nikupendaye) Hessed Hassad)

·      Atakuwa juu ya nyumba ya Mungu na Ufalme wa Mungu Milele.

Ukizitazama ahadi zote alizozitoa Mungu Je zinaendana na Sulemani? Bila shaka jibu ni hapana utawala wa sulemani haukudumu milele uliishia alipokufa sulemani,sulemani alipewa hekiman na ufahamu lakini huyu anayetajwa hapa amepewa kutawala juu ya Ufalme wa Mungu milele 

Bila shaka jambo hili ni muhimu bkujua ili kumtofautisha Mwana wa Daudi  aub Mfalme ajaye na Watoto wa Suylemani .

Kwa sababu pia huyu Mwana wa Daudi atakayezaliwa asili yake ni kutawala ufalme wa Mungu basi asili yake ni ya Uuungu pia Je Mwana Huyu ni nani?

Aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi ambaye ndiye Masihi aliyeahidiwa na Mungu na ana asili ya Uungu ni YESU KRISTO MWANA WA DAUDI pekee.

 

1NYAKATI 17:7-15

 “Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. 8 Nimekuwa pamoja nawe po pote ulipokwenda, nami nimewakatilia mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kama majina ya watu wengine wakuu sana wa dunia. 9 Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya hapo mwanzo, 10 na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israel. Pia nitawatiisha adui zenu wote.

Pamoja na hayo ninakuambia kwamba BWANA atakujengea nyumba: 11 Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kama mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake. 12 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. 13 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele, kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.

 

15 Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya. 

 

 

Yesu Kristo ni kutoka ukoo wa Ibrahimu

 

1.     Orodha ya Viuzazi kutoka Adamu mpaka Ibrahimu -watu walioshiba miaka duniani.Mwanzo 5 :1 

 

2.     Ahadi ya Mungu kwa ibrahimu Mwanzo 22:18 

 

‘’kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.’’

Kwa sababu ya utiifu wa ibrahimu kwa Mungu alipotaka kumtoa Isaka katika Mlima Moria Mungu anaahidi tena kwa abrahamu kuwa kupitia uzao wako ‘’ mataifa yote duniani yatabarikiwa…’’  Hapa tunaona kuwa huyu atakayezaliwa kila taifa duniani litabarikiwa, je ni baraka gani hiyon inayopita mataifa yote?Huyu atakayetoa hiyo Baraka ni nani?

  Katika taifa la Israeli ni uzao gani wa Ibrahimu ulikuwa baraka kwa mataifa yote? bila shaka tunaona mtembeo mkubwa wa taifa la Israeli kuwa liliyapiga vmno mataifda mengine na kuyamiliki ,Mtu pekee aliyetoka kwa Ibrahimu ni huyu aliyeahidiwa kutoka kwa Mungu na ana asili ya Uungu .

       Kwa sababu Mungu ni wa Baraka kwa watu wote (huwapa mvua wema na waovu)

                             Baraka ya Mungu haina mipaka

Je ni baraka gani ya Mungu iliyomwagika kwa watu wote? Bila shaka ni baraka ya wokovu kupitia Yesu Kristo Pekee.Yesu Kristo kwa Mujibu wa Kitabu cha Waefeso 1:3-8 inaonesha jinsi alivyotuneemesha na baraka =tele za kiroho 

 

*Wokovu ndiyo baraka Pekee na muhimu kutoka kwa ,Mungu  na akikupa haiondoi kamwe ndani ya Maisha yako.*