MATENDO YA MITUME
UTANGULIZI
Kitabu
cha Matendo ya Mitume kinaendeleza masimulizi ya Injili kadiri ya Luka.
Kitabu hiki kinaelezea jinsi ile jumuiya ya Kikristo aliyoanzisha Yesu
ilivyoongezeka tangu kufufuka kwake. Jamii hiyo iliendelea kukua hata
wakati mtume Paulo alipowasili Rumi akitangaza Habari Njema kwa uhodari
na bila kizuizi (Mdo 28:31).
Katika
kitabu hiki kuna sehemu nne ambazo mwandishi anatumia nafsi ya kwanza
wingi yaani (sisi) katika masimulizi yake: 16:10-17; 20:5-15; 21:1-18;
27:1—28:16. Sehemu hizi zote zinahusika na safari baharini na
zinaonekana kuwa ni kumbukumbu zilizowekwa na Luka juu ya matukio ya
siku kwa siku ya safari zake na msafiri mwenzake Paulo ambaye alikuwa
naye kule Filipi, Yerusalemu, Kaisaria, Antiokia (ambamo kwa mara ya
kwanza wafuasi wa Yesu wanaitwa “Wakristo”) (Mdo 11:2) na katika safari
ya kwenda Rumi.
Shabaha
ya Luka ni kumhakikishia Theofilo juu ya ukweli wa “mambo yote Yesu
aliyoyatenda na kufundisha” (Mdo 1:1-2; Lk 1:1-4) na jinsi Ukristo
ulivyoenea ulimwenguni kwa nguvu ya Roho Mtakatifu (1:8). Mwandishi
anahakiki kuwa Ukristo ni imani adili na kwamba vuguvugu hilo la Ukristo
halikuwa la uasi uliotishia dini ya Kiyahudi wala dola la Kirumi. Aidha
hakuna hata hakimu mmoja au wakuu wa serikali waliomsikiliza Paulo
ambao waliwagundua hao Wakristo kuwa na hatia yoyote ile.
Kwa
muhtasari kitabu hiki chaweza pia kuitwa, “Kitabu cha Matendo ya Roho
Mtakatifu” maana mada ya kudumu katika habari zake zote ni ile
inayoonesha jinsi nguvu ya Roho Mtakatifu ilivyowaimarisha na kuwasukuma
wanajumuiya wa kanisa changa. Kitabu cha Matendo ya Mitume chaweza pia
kuitwa “Kitabu cha Kwanza cha Historia ya Kanisa”, maana ndivyo kilivyo,
hatua kwa hatua.
Kitabu
hiki chaweza kugawanywa katika kile tunachoweza kuita “Hatua” tatu
kubwa, kulingana na vituo vya kijiografia vinavyohusiana na matukio
mbalimbali:
1. Hatua
ya kwanza: Yerusalemu (2:1—8:3). Baada ya Yesu kufufuka na kupaa
mbinguni (1:4-11) Yerusalemu ndicho kituo cha uumbikaji wa kiini cha
kale cha Ukristo (1:12-26). Hapo ndipo Roho Mtakatifu alipowashukia
mitume na wafuasi wa Yesu (2:4); hapo ndipo hatua za kwanza za muundo wa
kanisa zilipofanyika (2:41—8:3).
2.
Hatua ya pili: Yudea na Samaria (8:4—9:43). Tukio la kuwatesa Wakristo
lililoanza mara baada ya hotuba ya Stefano (6:9—7:60) liliwafanya wengi
wao kuondoka Yerusalemu na “kutawanyika katika nchi ya Yudea na Samaria”
(8:1). Tukio hilo lilisadia kuenea kwa Injili ambayo wakati huo ilikuwa
imeanza katika sehemu mbalimbali za Siria na Palestina (4:4-6,25-26;
9:19,30-32,35-36,38,42-43).
3.
Hatua ya tatu: kuenea kwa Injili mpaka miisho ya dunia (10:1—28:31).
Sauli wa Tarso alipokuwa katika kilele cha bidii yake ya kuwatesa
Wakristo, alipokuwa anakwenda Dameski, Mungu alimwita ili amfanye kuwa
chombo chake cha kuwaaplekea watu wa mataifa mengine Injili (9:15). Vile
vile wale waumini waliotawanyika kwa sababu ya mateso yale walienea
mpaka Foinike, Kipro na Antiokia (11:19) na kwa njia yao mlango wa
kuwafikia watu wengine na Injili ulifunguliwa. Kitabu kina masimulizi
juu ya safari tatu za mtume Paulo za kueneza Injili: tangu Asia Ndogo,
Europa kwa kupitia Makedonia na kufika Akaya (13:1—14:28; 15:36—18:22;
18:23—20:38). Mwishoni mwa safari yake ya tatu anarudi Yerusalemu
(21:1-15) ambapo alikamatwa hekaluni (21:27-30). Sura za mwisho zinaleza
mambo yaliyompata Paulo katika safari yake ya kwenda Rumi.
KWA KUSOMA ZAIDI UNAWEZA KUDOWLOAD KUONA JINSI INJILI NA UMISHENI VI;LIVYOENDELEA KATIKA SAFARI ZOTE TATU ZA UMISHENI
0 Comments
Post a Comment