*Nuru Huangaza gizani*


*Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.2 Wakorintho 4:6*


      *Nuru Huangaza gizani*

Neno Nuru Ina maanisha mwanga .Yesu ndiye Nuru inayozungumzia hapa kazi yake Ni kuangaza Moyoni mwetu ili kuondoa Giza ,na Giza Ni dhambi na uovu ambao hukaa Moyoni mwa Mtu .


Kama Maisha Yako yamegubikwa na sintofahamu jua upo gizani ,ujamwamini Yesu Kristo jua upo gizani,dunia inakuangaisha just Upo gizani .unahitaji Nuru imulike ili Giza liondoke maishani mwako .


kazi ya Nuru -Yesu Kristo katika Maisha yako Ni 


 🙌🏻kutoa Mwangaza MOYONI .

Mithali 4:23 inasema chemichemi za  Uzima zinatoka Moyoni na Kama kiza kimetanda au Mambo ya dhambi yametawala Moyo na nafsi yako jua Giza limetanda , Tafsiri ya Matendo Yako inaanzia Moyoni kilekile kilichojaza Moyo ndio kinatoa Mfumo wa Maisha na mawazo yako .*Mna Hila nyingi  Moyoni mwa Mtu..*


Yesu Kristo ndio Nuru na Mwangaza ukikiri na kumwamini anachokifanya anaweka msaidizi ndani yako (Roho Mtakatifu) ambaye ndiyo Mwangaza wa Milele kwako ambaye kazi Yake Ni kukumbusha kujitakasa kwa Kuamini Neno la Mungu linalokuasa Wewe kuacha dhambi.

Warumi 8.inazungumzia juu ya Kazi Yake Roho Mtakatifu Moja Ni *Kutusaidia kujua udhaifu wetu*.

Kama Aliyemwamini Kristo akitenda dhambi ndani yake Moto utawaka atajutia na kuumia Kabisa mpaka atubu ndipo Amani ya Kristo inakaa.


je umemwamini Kristo.Je Unatii Neno lake? Unaadibika linapokuadibisha? Je unawajibika linapotaka uwajibike?

Mungu atusaidie Sana.tuuone Mwangaza  wake. Moyoni mwetu.



🙌🏻inanipa Mwangaza wa Kumjua Mungu kwa kupitia Yesu Kristo


Jambo la Pili Yesu Kristo akiingia ndani Yetu Anatupa Uwezo wa kujua Maandiko Yake .Elimu Ni mafunzo na Mwangaza Ni Nuru Ni Sawasawa na Yesu Kristo pia Ni sawa na Roho Mtakatifu Aliyepo ndani Yetu.


kazi Ya Roho Mtakatifu Ni kutufundisha Sisi Neno na Kutusaidia kujua Siri za ufalme wa Mungu .


Yesu Kristo aliwaambia akiwajilieni Huyo Roho Mtakatifu atawajulisheni Mambo Yote 🙌 kumbe Ni Jambo la kujifunza Neno la Mungu kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu katika lile Neno .


Pia Biblia inatukunbusha kuwa 


Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.Matendo ya Mitume 5:32


Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake,Waebrania 3:7


Roho Mtakatifu yupo kwa Wamtiio Mungu wakiamini Jina lake Yesu na Wote wanaosikia Kutoka kwake hawapaswi kuwa na mioyo migumu ya kutobadilisha tabia zao 


je wajua Neno lake Mungu Ni Mwangaza ambao kazi take huweza kutukamilisha katika kutenda Mema kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

ndio Maandiko matakatifu yaasema .


*" 16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;2 Timotheo 3:16"*


*"17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.2 Timotheo 3:1"*



*Kiini Cha kusoma Biblia Ni Utii bila Utii hujajifunza na hujasoma tunajifunza kupitia kumsikiliza (Neno lake) na Kumtii Mungu*


Amini ,Tii,Tenda na Wambie wengine . Maandiko Matakatifu Ni Mwangaza kwa sababu hutuongoza katika Ukamilifu.


Amini Yesu ,Sikiliza (Soma) Neno la Mungu linasema Nini just yako,Tiii na Wambie wengine.


Nuru Ni Kristo Bwana wetu na Ayaangazie Maisha Yako leo na kukufadhili 🙏


*Mwamini  na Mkiri Yesu Kristo (Nuru) Akuondolee(akuangazie) dhambi (Giza)*


Karibu HKWYTANZANIA

Harakati ya kufanya wafuasi wa Kristo Tanzania .


Kutengeneza Wafuasi wanaofuasa wengine  

Namba ya kutuma Maombi ya kujiunga 076414161748.

jamesmalelesigala@gmail.com

Watu Kutoka mikoa Yote Mnakaribishwa kumbuka HKWYTANZANIA sio dhehebu Ni Huduma ya Hiari inayoshirikiana na kila Mtu Mwaminifu Ulimwenguni ili kueneza habari Njema ya Yesu Kristo.🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏